Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 27.01.2023

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Victor Osimhen

Manchester United inaweza kutoa ofa ya pauni milioni 105 kwa mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen lakini uhamisho wa mshambuliaji huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 23 huenda hautafanyika hadi msimu wa joto. (Soccer News - In Dutch)

 

United pia wanatazamia kuwatuma mshambuliaji wa Uingereza Charlie McNeill, 19, mlinzi wa Uholanzi Bjorn Hardley, 20, na mlinzi wa Uingereza Di'Shon Bernard, 22, kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la Januari. (Manchester Evening News)

 

Chelsea huenda ikalazimika kuchelewesha mipango ya kumsajili beki wa kulia wa Ufaransa Malo Gusto, 19, mwezi Januari huku rais wa Lyon Jean-Michel Aulas akisema anatarajia mchezaji huyo kusalia Ufaransa hadi angalau msimu wa joto. (Football London)

 

Tottenham wana imani kuwa dili la mlinzi wa Sporting Lisbon na Uhispania Pedro Porro litakamilika siku zijazo baada ya ugumu wa mazungumzo kuhusu kipengele cha kuachiliwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (90min)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tariq lamptey

Sporting wameuliza kuhusu kupatikana kwa Tariq Lamptey wa Brighton, 22, kuchukua nafasi ya Porro, huku Lyon pia ikimtaka beki huyo wa pembeni wa Ghana. (90min)

 

Everton wanatarajiwa kupunguza bei yao ya pauni milioni 60 kwa winga Mwingereza Anthony Gordon, 21, na kukubali karibu pauni milioni 40 pamoja na nyongeza baada ya hesabu yao ya awali kukataliwa na Newcastle. (Telegraph - subscription required)

 

Leeds wako tayari kulipa pauni milioni 25 kwa Juventus na kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 24. (Sky Sports Italy)

 

Bournemouth wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Roma na Italia Nicolo Zaniolo, 23, huku uhamisho wao wa kumnunua mshambuliaji wa Villarreal na Senegal Nicolas Jackson, 21, ukionekana kama umegonga mwamba. (Mail)

 

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Saint Maximin

AC Milan pia wanataka kumsajili Zaniolo lakini wanavutiwa na mshambuliaji wa Ufaransa na Newcastle Allan Saint-Maximin kama mbadala wake (Sky Sports Italy)

 

Chelsea, Newcastle na Manchester United wote wanavutiwa na mlinzi wa Uholanzi na Inter Milan Denzel Dumfries, huku Inter wakiweka bei ya euro 40m (ÂŁ35m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

 

Mshambulizi wa Blackburn Rovers Ben Brereton Diaz amekubali kujiunga na klabu ya La Liga Villarreal msimu wa joto kwa uhamisho wa bure. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile mwenye umri wa miaka 23 mkataba wake unamalizika Ewood Park mwishoni mwa msimu. (Mail)

 

Southampton wanamtaka winga wa Rennes na Ghana Kamaldeen Sulemana. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ndiye alikuwa mchezaji mwenye kasi zaidi kwenye Kombe la Dunia na hapo awali alikuwa akiivutia timu inayohangaika katika Ligi ya Premia Everton. (Mail)

.

Chanzo cha picha, bbcsport

Maelezo ya picha,

Cedric Soares

Leeds wanajipanga kumruhusu fowadi wao Muingereza Joe Gelhardt, 20, kujiunga na Sunderland inayosaka Ubingwa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Sky Sports)

 

Fulham wameripotiwa kukubali mkataba wa mkopo kwa beki wa pembeni wa Arsenal na Ureno Cedric Soares, 31. (90min)

 

Arsenal wanajaribu kusajili kiungo kabla ya dirisha kuisha, huku mchezaji wa Everton na Ubelgiji Amadou Onana, 21, akiwa chaguo. (Express)

 

Fiorentina hawataki kumruhusu Sofyan Amrabat, 26, kuondoka katika dirisha la usajili la Januari baada ya kiungo huyo wa Morocco kuvutia Liverpool na Tottenham wiki za hivi karibuni. (90min)