Maisha ya Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico hayako hatarini tena (naibu waziri mkuu)
Pata taarifa kuu

Maisha ya Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico hayako hatarini tena (naibu waziri mkuu)

Maisha ya Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico hayako hatarini tena, hata kama hali yake bado ni mbaya, Naibu Waziri Mkuu Robert Kalinak ametangaza kwa vyombo vya habari Jumapili, Mei 19, siku nne baada ya shambulio ambalo mkuu wa serikali ndiye alikuwa mlengwa. 

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico anawasili kwa mkutano wa V4 huko Prague, Jamhuri ya Czech, Jumanne, Feb. 27, 2024. Ripoti za vyombo vya habari zinasema Jumatano, Mei 15, 2024 kwamba Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico alijeruhiwa kwa risasi na kupelekwa hospitalini.
Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico anawasili kwa mkutano wa V4 huko Prague, Jamhuri ya Czech, Jumanne, Feb. 27, 2024. Ripoti za vyombo vya habari zinasema Jumatano, Mei 15, 2024 kwamba Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico alijeruhiwa kwa risasi na kupelekwa hospitalini. AP - Petr David Josek
Matangazo ya kibiashara

"Hakuna tena hatari yoyote ya haraka kwa maisha yake, lakini hali yake bado ni mbaya na anahitaji uangalizi maalum," amesema Bw. Kalinak, mshirika wa karibu wa kisiasa wa Robert Fico.

Waziri Mkuu amelazwa hospitalini tangu Jumatano, wakati mtu mmoja alipomfyatulia risasi na kumpiga mara kadhaa, haswa tumboni. Alifanyiwa upasuaji wa saa tano siku ya Jumatano na mwingine mfupi zaidi siku ya Ijumaa, katika hospitali moja katika mji wa Banska Bystrica katikati mwa Slovakia.

Mshambuliaji huyo aliyetambuliwa na vyombo vya habari vya Slovakia kuwa mshairi Juraj Cintula mwenye umri wa miaka 71, alimfyatulia risasi tano Robert Fico na kumpiga mara nne.

Mtu anayezuiliwa na anayeshukiwa kumpiga risasi Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico ni Juraj Cintula, mzee wa miaka 71 kutoka katikati mwa nchi, aliyetambuliwa na vyombo vya habari vya Slovakia kama mwandishi wa ndani.
Mtu anayezuiliwa na anayeshukiwa kumpiga risasi Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico ni Juraj Cintula, mzee wa miaka 71 kutoka katikati mwa nchi, aliyetambuliwa na vyombo vya habari vya Slovakia kama mwandishi wa ndani. © DR

Aliwasilishwa Jumamosi mbele ya mahakama ya jinai huko Pezinok, kaskazini mashariki mwa Bratislava, ambayo iliamuru abaki kizuizini kabla ya kesi.

Bw. Fico, mwenye umri wa miaka 59, alirejea kwenye wadhifa wa Waziri Mkuu msimu uliopita, kwa muhula wa nne, baada ya chama chake, Smer-SD, kushinda uchaguzi wa wabunge.

Alifanya kampeni haswa juu ya mapendekezo ya amani kati ya Urusi na Ukraine, nchi jirani ya Slovakia, na juu ya kusitisha msaada wa kijeshi kwa Kyiv, ambayo serikali yake ilitekeleza.

Nchi iliyogawanyika

Jaribio hilo la mauaji liliishtua sana Slovakia, nchi yenye wakazi milioni 5.4, mwanachama wa Umoja wa Ulaya na NATO, ambayo imegawanyika vikali kisiasa kwa miaka mingi.

Rais anayeondoka anayeunga mkono Magharibi, Zuzana Caputova, na mrithi wake, Peter Pellegrini, mshirika wa Bw. Fico ambaye atachukua madaraka mwezi Juni, walitoa wito kwa raia wenzao kujiepusha na "makabiliano" yoyote baada ya tukio hilo.

Pia waliitisha mkutano wa viongozi wote wa vyama vya bunge Jumanne ili kuonyesha umoja kufuatia shambulio hilo, huku Bi Caputova akibainisha kuwa nchi hiyo inahitaji "maridhiano" na "amani".

Lakini migawanyiko hauonekani kuwa karibu na utulivu. Bw. Kalinak mara moja alipendekeza kuwa Smer-SD haitashiriki katika mkutano huu ulioitishwa huku "kiongozi wetu (wa chama) yuko mikononi mwa madaktari".

Na baadhi ya wanasiasa wa Slovakia tayari wametoa shutuma dhidi ya wapinzani wao, wakiwatuhumu kuwa nyuma ya shambulio hilo.

Bw. Kalinak mwenyewe aliwakosoa wanasiasa wa upinzani na baadhi ya vyombo vya habari siku ya Ijumaa kwa kueleza, kabla ya jaribio la mauaji, Bw. Fico kama mhalifu, dikteta au mtumishi wa Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Na viongozi kadhaa wa vyombo huru vya habari walisema walianza haraka sana baada ya shambulio hilo kupokea vitisho kutoka kwa wasomaji, na kulemewa na shutuma kutoka kwa washirika wa kisiasa wa Bw. Fico.

Kufichuliwa na vyombo vya habari vya Kislovakia mwaka wa 2018 kuhusu uhusiano kati ya serikali ya Bw. Fico na mafia wa Italia kulizua sintpofahamu, huku kukizuka maandamano makubwa zaidi tangu kuanguka kwa ukomunisti, na hatimaye kumlazimisha Bw. Fico kujiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.